Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Nyandarua MCA

MCA wa 2097 Amefika

Siku hizi, ukisimama mbele ya wananchi ukisema unataka kuwa MCA, maswali ni mengi kuliko ya KCPE! Wananchi wanataka MCA wa aina gani? Elimu: Unaelewa kazi ya MCA au umeamka tu ukajiona uko tayari kuongoza? Maendeleo: Umeleta nini kwa wananchi, ama maendeleo yako ni picha za Facebook pekee? Uadilifu: Pesa za umma zikifika mikononi mwako, utazitumia kwa maendeleo ama tutaanza kusikia hadithi za “system iko down”? Uwakilishi: Utatetea wananchi katika Bunge la Kaunti, ama utakuwa wa kusema “ndio, mheshimiwa” kila siku? Ufikivu: Baada ya uchaguzi, simu yako itakuwa inaita kweli, ama itaanza kuita tu wakati wa kampeni? Maono: Una mpango wa kuboresha huduma za afya, barabara, maji na nafasi za vijana, ama slogan yako ni “tutafanya”? Na muhimu zaidi, MCA si mfadhili wa kila mtu binafsi. Kazi yake ni kutunga sheria za kaunti, kuwakilisha wananchi, kushiriki kuidhinisha bajeti na kuisimamia serikali ya kaunti. Kwa hiyo, tunahitaji mtu anayejua wajibu wake na anayewajibika kwa wananch...